September 26, 2020




 FRANK Lukwaro, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania amesema kuwa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini lipo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa leo Septemba 26 dhidi ya Dodoma Jiji.

 Timu hizi mbili zinakutana leo uwanjani kila mmoja akiwa na uhitaji wa kupata pointi tatu muhimu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ndani ya ligi ambayo imeanza kwa kasi msimu wa 2020/21.

Polisi Tanzania inakutana na Dodoma FC iliyo nafasi ya nne na pointi zake saba baada ya kucheza mechi tatu. Polisi Tanzania yenyewe ipo nafasi ya 9 na pointi 4 kwenye msimamo wa ligi.

Mechi ya Polisi Tanzania iliyopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania huku Dodoma FC ikilazimisha sare ya bila kufungana na Coastal Union, Mkwakwani, Tanga.

Lukwaro amesema:"Mipango ipo sawa na hakuna tatizo katika maandalizi yetu kikubwa tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu wa leo.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu ila haina maana kwamba tutashindwa kuleta ushindani hapana lazima tushindane ili kupata matokeo mbele ya wapinzani wetu leo.

"Kwa mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi na kuipa sapoti timu yao kwa kuwa kila mmoja anatambua kwamba tupo kwenye ushindani na tunahitaji matokeo."



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic