INTER Milan ipo kwenye mpango wa kuipata saini ya kiungo wa Chelsea raia wa Ufaransa, N'Golo Kante msimu huu licha ya kukutana na vigingi kutoka kwa mabosi wake.
Antonio Conte alishinda taji la Ligi Kuu England akiwa na Kante wakati alipokuwa ndani ya Chelsea hivyo anakubali uwezo wake na anajua namna ya kumtumia iwapo atampata ndani ya Klabu ya Inter Milan.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia zimeeleza kuwa ili Inter Milan waipate sani ya nyota huyo ni lazima wamuuze mchezaji wao mmoja ili kufikia malengo ya dau la nyota huyo ambalo linatajwa kuwa ni Euro milioni 46.
Chelsea hawana mpango wa kumuuza nyota huyo kwani walipokea ofa ambayo iliwahusisha wachezaji wawili ambao ni Christian Eriksen and Marcelo Brozovic.
Miamba hiyo ya Italia inahitaji saini ya Kante mwenye miaka 28 ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao ambacho kinahitaji kufikia mafanikio makubwa kwa msimu wa 2020/21.
Chelsea wapo tayari kumuuza nyota wao Jorginho kuliko Kante na hawana habari na wachezaji wawili ambao wameambiwa watapewa ikiwa ni Eriksen ama Brozovic.
0 COMMENTS:
Post a Comment