September 28, 2020

 


ABDALAH Mohamed, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


JKT Tanzania inaingia uwanjani kupambana na Coastal Union ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania.


Mohamed amesema""Tunajua kwamba tutakuwa ugenini na Coastal Union wao wapo nyumbani kwao Uwanja wa Mkwakwani hilo halitupi shida.


"Tumejipanga na kikosi kipo vizuri kwa ajili ya kupata pointi tatu kwani kila kitu kipo sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya ligi.


"Kukosa matokeo kwenye mechi yetu iliyopita haina maana kwamba tutashindwa kupata matokeo hapana tupo tayari na mashabiki watupe sapoti, tumejipanga kwa ajili ya mechi zote bila kujali tunacheza na nani hata iwe Namungo."


Mchezo wa leo ni wa raundi ya nne utapigwa majira ya saa 10:00 jioni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic