September 13, 2020


 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong amesema kuwa sababu kubwa ya kushangilia kwa kushika macho na kuweka mkono kifuani ni imani kwamba kufunga kwake mabao inatokana na uwezo wa Mungu.

Sarpong ametupia mabao mawili Bongo na wakati wa kushangilia kila akifunga bao amekuwa akishika macho kufuatia kufanya hivyo katika mechi mbili alizofunga tangu ajiunge na timu hiyo.

 

Mshambuliaji huyo amejiunga na Yanga akitokea Rayon Sport ya nchini Rwanda ambapo alifanikiwa kufunga mabao 30 katika misimu miwili aliyoweza kucheza kabla ya kujiunga na Yanga ambapo hadi sasa tayari amefunga mabao mawili katika mechi mbili alizocheza.


Alifunga kwenye mechi ya kitaifa ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir na ya pili ilikuwa ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, zote ni Uwanja wa Mkapa.


“Nashukuru napata nafasi ya kufunga kwangu ni jambo kubwa lakini hii inatokana na ushirikiano wa timu nzima ambayo tumekuwa tukipambana.


“Unajua kushangilia kule huwa namaanisha kwamba kufunga kwangu mabao siyo uwezo wangu bali ni Mungu ndiyo anasababisha nafunga wala hakuna jambo lingine zaidi ya hilo,” amesema Sarpong.


Leo Yanga ina kazi ya kumenyana na Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Amri Said, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00, usiku.

2 COMMENTS:

  1. Sawa leo piga 3 ili viongoz wa Simba wakae kikao

    ReplyDelete
  2. Kuna watu watajisifu wakishinda Leo lakini hawajui Ni sawa Na kupiga bomu mochwari Na kujisifu umeua.Kumbukumbu KMC 4 Mbeya City 0.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic