KIKOSI cha Mwadui FC kinachonolewa na Khalid Adam leo kimeibuka na ushindi kwa mara ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 kwa kuambulia kichapo mechi zote.
Leo, Septemba 27 imeshinda mabao 2-0 mbele ya Ihefu FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Mabao ya ushindi yalipachikwa na Fred Felix dakika ya 6 na Wallace Kiango dakika ya 37 na kuwafanya wamalize dakika 45 za mwanzo wakiwa mbele kwa mabao hayo mawili.
Kipindi cha pili dakika 45 zikikuwa ngumu kwa timu zote mbili ambapo hakuna timu iliyoona lango la mpinzani wake, Mwadui walikwama kuongeza bao huku Ihefu FC nao wakikwama kuweka mzani sawa.
Mechi za mwanzo ilikuwa namna hii kwa Mwadui walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United, wakapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Dodoma Jiji na kete yao iliyopita ilikuwa ni mbele ya KMC ambapo walinyooshwa mabao 2-1.
Ihefu pia nao wameanza kwa kusuasua ambapo walianza kwa kupoteza mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 2-1 kisha wakashinda mbele ya Ruvu Shooting bao 1-0 walichapwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar na leo wamepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Mwadui FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment