September 27, 2020

 




FT:Mtibwa Sugar 0-1 Yanga

Jamhuri, Morogoro

Yanga inasepa na pointi tatu jumlajumla baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu hiyo kushinda bao 1-0 lililofungwa na Lamine Moro.

Dakika ya 88 Yanga bado wapo mbele kwa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri

Mtibwa Sugar 0-1 Yanga

Goaaal dakika ya 61 Lamine Moro anafunga kwa Yanga ndani ya 18 kwa kona ya Carlos


Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Jamhuri

HT: Mtibwa Sugar 0-0 Yanga

Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mpira kwa sasa Uwanja wa Jamhuri ni mapumziko.Yanga wameweza kwenda mapumziko takwimu zikionyesha kuwa wamekuwa na umiliki wa mpira asilimia 52 huku Mtibwa Sugar wakiwa na asilimia 48.


Kwa upande wa kona, Yanga imepiga jumla ya kona tatu huku Mtibwa Sugar ikipiga kona mbili.


Mchezo umekuwa ni wa nguvu nyingi kwa pande zote ambapo Mtibwa Sugar imecheza jumla ya faulo 13 na Yanga imecheza faulo 7.

Mashuti yasiyolenga lango, Yanga imepiga jumla ya mashuti matatu sawa na Mtibwa Sugar


Timu zote mbili, Mtibwa Sugar ambao ni wenyeji pamoja na Yanga ambao ni wageni kwenye mchezo wa leo wa raundi ya nne hakuna ambaye ameona lango la mpinzani.


Dakika 45 zilikuwa ni za ushindani mkubwa ambapo kila timu imeonekana inapambana kupata bao kwa mpinzani mwenzake.


Mtibwa Sugar 0-0 Yanga

Uwanja wa Jamhuri,Morogoro

UWANJA wa Jamhuri Morogoro kwa sasa ni mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara raundi ya nne.


Kipindi ni cha kwanza kwa sasa Uwanja wa Jamhuri

Ushindani ni mkubwa kwa timu zote mbili ambapo kila timu inapambana kusaka pointi tatu muhimu.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic