ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.
Rekodi zinaonyesha kuwa kwa misimu miwili mfululizo ambayo Azam FC imekutana na Tanzania Prisons mechi zao zilikuwa kali na zenye ushindani mkubwa.
Msimu wa 208/19 Azam FC iliweza kupata ushindi mara moja sawa na Tanzania Prisons ambapo timu zote zilishinda kwenye mechi zao za nyumbani kwa ushindi wa bao 1-1.
Msimu wa 2019/20 kwenye mechi mbili wakati wakisaka pointi sita wote wawili waligawana pointi mojamoja baada ya kutoshana nguvu.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine ngoma ilikamilika kwa kufungana mabao 2-2 kisha mara ya pili walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Uhuru.
Leo wanakutana kwa mara ya kwanza Uwanja wa Nelson Mandela kwa msimu wa 2020/21 ambapo timu zote zimetoka kushinda mechi zao zilizopita.
Azam FC ikiwa ugenini ilishinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City na Tanzania Prisons ilishinda bao 1-0 mbele ya Namungo FC.
Thabit amesema:"Hautakuwa mcheozo mwepesi kila timu inahitaji ushindi hata sisi tunahitaji ushindi pia na kwa namna wapinzani wetu tutapambana kupata ushindi."
0 COMMENTS:
Post a Comment