October 14, 2020



SERGIO Aguero nyota wa Klabu ya Manchester City ambaye anacheza timu ya Taifa ya Argentina amesema kuwa alikuwa akimkasirisha nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa kuwasha TV usiku kucha jambo lilikuwa linamkasirisha nyota huyo .

Aguero na Messi wamekuwa marafiki ndani ya timu Taifa ya Argentina na Messi amekuwa ni mwalimu kwa Arguero kwenye makosa yake anayoyafanya mara nyingi wanapokuwa kambini.

Aguero amesema kuwa alikuwa anapenda kulala huku akiacha TV wazi na wakati mwingine kushinda akiongea na simu jambo ambalo Messi alikuwa akimlalamikia.

Wamecheza kwa pamoja kwenye mashindano makubwa ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia mara tatu na mara nne Copa America na walishinda taji la dhahabu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Beijing Olympics.

Muda wote huo walikuwa ni marafiki pia walikuwa wakilala chumba kimoja jambo ambalo lilimfanya Aguero awe na furaha wakati Messi alipokuwa akihusishwa kujiunga na Manchester City kabla ya dili lake kuyeyuka mazima msimu huu. 

"Muda wote amekuwa ni mtu wa kulalamika hasa pale ambapo ninafanya makosa kwani tulipokuwa chumbani nilikuwa napenda kutazama TV usiku mpaka ninasinzia na nikiamka tu asubuhi alikuwa analalamika kwangu.

"Muda mwingine amekuwa akiamka na kuondoka kwenda kufanya mazoezi ila mimi nilikuwa ninakaa ndani huku ninaongea na simu kisha anarudi kwangu na kuniambia kwamba ni muda wa kula ama kufanya mazoezi kwa kuwa hatuna muda," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic