October 14, 2020

 


IMEBAINIKA kuwa wakati Mrundi Cedric Kaze, akijiandaa kuja kuchukua mikoba ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Waholanzi ndiyo ambao watahusika kumleta kocha huyo hapa nchini.

 

Waholanzi hao kupitia Shirika la Ndege la taifa hilo, KLM Royal Dutch Airlines (KLM), ndiyo watakaombeba Kaze kwa kumtoa Canada alipo kwa sasa na kumshusha katika ardhi ya Tanzania Alhamisi saa 4 usiku, maalum kuanza kazi kwenye kikosi hicho.

 

Kaze anatua Bongo kwa ajili ya kuungana na Yanga baada ya timu hiyo kusitisha mkataba wa Mserbia, Zlatko Krmpotić ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

 

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema ndege hiyo ya KLM ndiyo ambayo itahusika kumshusha kocha huyo hapa nchini. “Kocha atafika na ndege ya KLM, siku ya Alhamisi saa 4 usiku kwa ajili ya kuanza kazi,” alisema kwa kifupi Hersi.


Kwa sasa Yanga ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi inajiandaa na mechi zake za Ligi Kuu Bara ambapo mchezo wake unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya Polisi Tanzania.


Mchezo huo utachezwa Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa utakuwa ni wa sita kwa Yanga iliyo nafasi ya tatu na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.

7 COMMENTS:

  1. Huku kuripoti ni ukanjanja haswa.

    ReplyDelete
  2. Siku hazigandi. Hebu Alhamis ifike tuone na itokee kweli ili wana Yanga tushushe presha zetu kwa sababu si kwa kumsifia huku

    ReplyDelete
  3. unaandika kama kwamba amekodi ndege na ni yeye tu ndiyo atakuwa abiria pekee katika ndege ya KLM
    umbumbumbu ule ule unarudiwa... Eymayel alisajiliwa akawa anatambulishwa kwamba aliipa ubingwa TP Mazembe...mwaka 2010 wakati current records zilikuwa zinaonyesha alivyokuwa anavurunda South Africa..

    huyu tunatambulishwa kwamba alikuwa kocha bacerona..kumbe pale alikuwa anafanya kazi tuu. ndiyo alikuwz kocha bora East Africa 2013....na kuanzia hapo amefanya nini..

    kwa kuwa mchezaji kaifunga TZ kasajiliwa...tulikuwa tunasikia eti Onyango ni babu..Sasa tambueni huyo mchezaji ana umri zaidi ya hamisi Tambwe na ni babu kweli

    acheni umbumbumbu na utopolo

    ReplyDelete
    Replies
    1. soka letu bongo ni la magezetini.Wanavyomsifia na kumpa kick huyu kocha utafikiri anakuja kuleta maajabu ya Bayern Munich kuifunga Barcelona goli 8.
      Kufundisha Academy ya U12 siyo muziki wa kuwafundisha kina Saidi Ntibazonkiza wa umri miaka 35.Ningewaelewa kidogo kama wangemrudisha Babu Hans Pluijm au Lwandamina.Mwandishi jaribu kuwa na uweledi kidogo ktk kuhabarisha na sio kutuletea hizi pumba za kupanda ndege ya KLM.

      Delete
  4. Mikia bhana kocha anakuja yanga nyie mnawashwa nin

    ReplyDelete
  5. Nguruwe fc tulia dawa iwaingie vizr

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic