ARSENAL inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta imekamilisha dili la nyota wa Atletico Madrid, kiungo Thomas Partey raia wa Ghana.
Washika bunduki hao ambao msimu wa 2020/21 wameanza vema na mchezo wao uliopita ndani ya Ligi Kuu England dhidi ya Sheffield United ilishinda kwa mabao 2-1 inahitaji kuwa tofauti zaidi kwa kujiboresha.
Ina kibarua cha kumenyana na Manchester City, Oktoba 17 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Inaelezwa kuwa dau la kiungo huyo ni Euro milioni 45 ambazo zimetumika kumnunua nyota huyo mwenye miaka 27.
Arteta amesema kuwa:"Nilikuwa ninamfuatilia Partey kwa muda mrefu na ninaamini kwamba kufika kwake hapa kutakuwa na maana kubwa, na atafanya vizuri."
0 COMMENTS:
Post a Comment