MBWANA Samatta, nahodha wa timu yaTaifa ya Tanzania amewaomba wanaoandika mambo yasiyo mazuri katika ukurasa wa timu yake mpya Fenerbahce kuacha kufanya hivyo.
Samatta amesistiza kwa kwa wale wanaofanya hivyo wanatia ugumu hata kwa Watanzania wengine huko mbele kupata timu kwa kwa kuwa timu zitakumbuka kuhusu wachezaji wa Kitanzania.
Alipokuwa akicheza Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England baadhi ya mashabiki walikuwa wakienda kwenye ukurasa rasmi wa timu hiyo na kuandika maneno ambayo yalikuwa hayaleti picha nzuri wakilalamika kwamba alikuwa ananyimwa pasi ili asifunge.
Hatua hiyo ilimfanya Samatta kuomba mashabiki wa Tanzania kuacha kuandika ujumbe usiofaa na waliweza kumsikia nahodha huyo ambaye ana kazi ya kukiongoza kikosi cha Taifa Stars Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Burundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment