CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kikosi kipo kamili leo kumalizana na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Christina amesema kuwa wanaamini mchezo wa leo watashinda kwa ushindi mkubwa kama ambavyo walianza mbele ya Mbeya City waliposhinda kwa mabao 4-0.
Christina amesema:"Tupo salama na maandalizi ya mwisho yapo vizuri hivyo mashabiki watupe sapoti na wajitokeze kwa wingi kuona namna gani wanaweza kutupa sapoti ili kushuhudia namna tutakavyopata ushindi.
"Leo tunarejea nyumbani kwa ajili ya kuendelea na mechi yetu ya ligi kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani ya kweli na burudani kutoka kwa wachezaji ambao wapo tayari kutupa ushindi."
KMC inashuka uwanjani kukutana na Polisi Tanzania ambayo imetoka kushinda mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji na KMC imetoka kupoteza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa bao 1-0.
Mchezo wa leo ni wa mwisho kukamilisha raundi ya tano ndani ya ligi kabla kwa msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment