October 11, 2020


 AZAM FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wanaendelea kukinoa kikosi kwa ajili ya muendelezo wa kutoa burudani kwa mashabiki wake na jana, Oktoba 10 walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili licha ya Azam FC kushinda kwa mabao 3-1.


Kwa sasa Azam FC ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 15 baada ya kucheza mechi 5 ina kibarua cha kucheza na Mwadui FC, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 15.


Awali ulipaswa uchezwe Oktoba 9 kutoka na mapumziko yaliyotokana na mechi za kimataifa umepelekwa mbele na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Nafasi ya pili ipo mikononi mwa Simba huku nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Yanga zote zina pointi 13 baada ya kucheza mechi tano, zimeshinda nne na kulazimisha sare mechi mojamoja.


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa na wataendelea kupambana ili kupata matokeo chanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic