ZLATKO Krmpotic, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga licha ya kufungashiwa virago ndani ya kikosi hicho huku nafasi yake ikitajwa kuzibwa na Cedric Kaze, kocha huyo ameandika rekodi yake ndani ya ardhi ya Bongo.
Rekodi ya kwanza ni kuwa Kocha Mkuu wa kwanza ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 kufutwa kazi mazima ndani ya mwezi Oktoba akiwa ni kinara wa ligi kwa sababu aliposhinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union timu yake ilipata muda mfupi wa kuongoza kabla ya Azam FC kushinda mabao 4-2 mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Azam Complex.
Kocha huyo alifungashiwa virago akiwa ameongoza timu yake kukusanya pointi 13 na kufunga mabao saba huku akifungwa bao moja na kwenye mechi zote zile za mikoani alipeta kwa kukusanya pointi tisa kwa kuwa aliongoza kikosi chake kucheza mechi tatu ugenini na alishinda kwa bao mojamoja mechi zote.
Rekodi nyingine ambayo kocha huyo ameandika ndani ya Bongo ni jina lake kuingia fainali za kuwania kocha bora wa mwezi Septemba akipigana vikumbo na Sven Vandenbroeck wa Simba pamoja na Aristica Cioaba wa Azam ambaye ametwaa tuzo hiyo.
Aliwasili nchini Agosti 29 na kufutwa kazi Oktoba 3 amekaa ndani ya ardhi ya Bongo kwa muda wa siku 36 na ameondoka akiwa hajapoteza mchezo hata mmoja.
Kocha wa pili kufutwa kazi kwa mwezi Oktoba alikuwa ni Maka Mwalwisi wa Ihefu ambaye alikuwa na mwendo wa kusuasua kwenye bechi lake la ufundi.
Alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi tano na alishinda mechi moja na kupoteza mechi nne na kumfanya ajikusanyie pointi 3 kibindoni.
Ww mwandishi wa habar n chiz kwel,,yanga amecheza mechi gan 3 za ugenini? Kama sio uongo mtupu
ReplyDeleteKapitiwa tu kdgo
ReplyDeleteTutumie lugha za ustaha, amecheza mechi 2 ,mtibwa na kagera, lakini kukosea kusikokuwa na madhara ni bora kuliko lugha zisizo na staha, kumradhi tuna rekebishana tu
ReplyDeleteHahahaha hatari
ReplyDelete