BEKI kisiki ndani ya Klabu ya Kagera Sugar, David Luhende ameingia kwenye anga za mabeki wageni wanaokipiga ndani ya Simba na Yanga kwa kuwa miongoni mwa waliofungua akaunti za mabao msimu wa 2020/21.
Lamine Moro wa Yanga ni kinara kwa watupiaji ndani ya Bongo kwa upande wa mabeki ambapo kibindoni ana mabao mawili kwenye ligi aliwafunga Mbeya City Uwanja wa Mkapa na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Beki mwingine ni Pascal Wawa wa Simba ambaye alimtungua kipa wa Gwambina FC Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 3-0.
Luhende ambaye msimu wa 2019/20 aliingia tatu bora kwenye msako wa beki bora wa msimu akiwa na rekodi ya kucheza mechi zote 38 za ligi na kutumia dakika 3,420, alianza kwa kutoa pasi ya kwanza mbele ya KMC wakati timu yake ikishinda bao 1-0 lililofungwa na Yusuph Mhilu.
Alifunga bao lake la kwanza wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-2 Uwanja wa Azam Compelex na kumfanya awe anga za mabeki wa Simba na Yanga kwa kutupia.
Kwa sasa Kagera Sugar inajipanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 14, Uwanja wa Majaliwa.
Vizur kijana
ReplyDelete