October 12, 2020

 


KLABU ya Yanga ndani ya mwezi Oktoba ina mechi tatu za moto ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mechi hizo ndani ya dakika 270.


Ikiwa mchezo wake ule wa dabi dhidi ya Simba ambao ulitarajiwa kuchezwa Oktoba 18 kupelekwa mbele mpaka Novemba 7 sasa itaanza namna hii:-

Yanga dhidi ya Poisi Tanzania Uwanja wa Mkapa, Oktoba 22, timu zote zimetoka kushinda mechi zao zilizopita.


Yanga ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania ilishinda mbele ya KMC bao 1-0.

KMC v Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba itakuwa Oktoba 25.


Wenyeji KMC wametoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania huku Yanga ikiwa imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union.

Biashara United v Yanga, Oktoba 30.


Kigongo cha mwisho kwa Yanga, Oktoba 30 itakuwa ni dhidi ya wanajeshi wa mpakani, Biashara United ambao wao wametoka kushinda mbele ya Mtibwa Sugar bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic