October 16, 2020

 


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Oktoba 16 wa mzunguko wa sita kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Jamhuri Dodoma umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ya bila kufungana.

Kwa Mbeya City unakuwa mchezo wake wa sita mfululizo kushuka uwanjani na safu yake ya ushambuliaji inatoka uwanjani bila kuambulia bao.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi zake mbili baada ya kupata sare mbili na zote ilikuwa ni 0-0.

Pointi ya kwanza ilikusanya ikiwa pale Uwanja wa Sokoine ambapo ilitoshana nguvu na Tanzania Prisons na leo imetoshana nguvu na Dodoma Jiji ya Mbwana Makatta.

Dodoma inafikisha jumla ya pointi 11 ikiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na kinara ni Azam FC ina pointi 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic