NAHODHA wa Simba ambaye ni mfungaji mzawa mwenye mabao zaidi ya 100 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa mtaalamu wa viungo ndani ya timu hiyo, Paulo Gomez.
Bocco alipata majeraha ya enka kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Simba ilipokubali sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Nyota huyo Oktoba 8 aliondolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Burundi uliochezwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa ili atengamae afya yake.
Mchezo huo ulikamilika kwa Stras kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa Bocco anaendelea salama kwa sasa kwa kuwa ameshaanza kufanya mazoezi mepesi.
0 COMMENTS:
Post a Comment