PRINCE Dube, jana Oktoba 12 alikiongoza kikosi chake cha Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Bao la kwanza kwa Azam FC lilipachikwa na kiungo Mudathir Yahya dakika ya 24 dakika ya 43 Dube ambaye alifunga mabao mawili alipachika bao lake la kwanza kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Azam FC kuwa mbele kwa mabao 2-0.
Bao lake la pili alipachika dakika ya 44 na kufanya Azam FC kuwa mbele kwa mabao 3-0 mpaka muda wa mapumziko na Fountain Gate ambao wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza walikwama kupata bao la kufuta machozi.
Msumari wa mwisho ulipachikwa na Kader dakika ya 49 na kuipa ushindi timu yake hiyo Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya timu zote mbili kuwekana sawa kwa kuwa Azam FC inajiadaa na mechi zake za Ligi Kuu Bara huku Fountain ikijiandaa na mechi za Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment