October 13, 2020


 KIUNGO wa Klabu ya Chelsea raia wa Ufaransa, N'Golo Kante anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo mwezi Januari baada ya kuzozana na Kocha Mkuu, Frank Lampard baada ya kugomea kumpa ruhusa ya kwenda kwenye sherehe ya ndoa ya rafikiye kwa mujibu wa ripoti.

Kiungo huyo ambaye ni miongoni mwa wanaofanya vizuri duniani kwa sasa na ndani ya timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwa sasa yupo kwenye majukumu yake ya timu ya taifa.

Ripoti zinaeleza kuwa Lampard aligomea ishu ya Kante kuacha mafunzo kwa muda na kuhudhuria sherehe ya harusi ya rafikiye kabla ya mapumziko mafupi yaliyotokana na timu za taifa kuwa kwenye majukumu.

 

Kiungo huyo mwenye miaka 29 ripoti zinaeleza kuwa anaweza kuibukia ndani ya Klabu ya Real Madrid ambayo inashiriki La Liga kwa kuwa ni timu ambayo anaipenda iwapo ataondoka ndani ya Stamford Bridge 

Kante hakuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake mwanzoni mwa msimu kwa kuwa alianza kukaa karantini kutokana na hofu ya kwamba ana maambukizi ya Virusi vya Corona.

1 COMMENTS:

  1. Huyu Lampard ataiharibu chelsea, Kante sio mtu wa kumwekea mizengwe, ni mstaarabu mno

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic