KIKOSI cha Simba kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Oktoba 12 kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya Ndanda FC.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Azam Complex saa 11:00 jioni na kiingilio kwa mzunguko ni buku saba, (7,000).
Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa sasa wanakiandaa kikosi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kesho watafanya mambo makubwa kwa kutoa burudani kwa mashabiki pamoja na kupata matokeo mazuri.
"Tunakwenda kufanya mambo makubwa na tutatoa burudani kwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona burudani na kushuhudia ushindi mzuri.
"Hatuchezi tu ilimradi tunacheza bali tunacheza na kutoa burudani. Simba ni timu ambayo inakupa burudani na kukupa matokeo, mashabiki mjitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu," amesema.
Ndanda inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa inapambana kurejea Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Mchezo wake wa kwanza dhidi ya African Lyon ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment