OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi leo Uwanja wa Azam Complex kushuhudia burudani na gongagonga zitakazotolewa kutoka kwa wachezaji wao.
Leo Simba itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa saa 11:00 jioni ambapo kiingilio kwa mzunguko ni shilingi 7,000, (buku saba).
Manara amesema:"Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani kuanzia wale wa makazi ya Chamazi, Kigamboni, Mbagala wanapaswa watambue kwamba mabingwa wa nchi Simba watashuka uwanjani kucheza dhidi ya Ndanda FC.
"Mechi hii ukiikosa utajitakia magonjwa kwani tutapiga mpira wa visukarisukari na ni uwanja mzuri tunakwenda kucheza sasa sijui unahitaji nini sasa hapo.
"Najua mnatambua kwamba kuna wachezaji wengi wazuri ndani ya Simba hivyo hakuna ambaye hajui namna timu yetu inavyofanya muda wote uwanjani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment