October 13, 2020


WINGA Saidi Ntibazonkiza anayekipiga timu ya Taifa ya Burundi ambaye amesaini dili la mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu ya Yanga ataanza kutumika rasmi Novemba 15.


Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuanza kutumika Novemba 15 ni kutokana na kutimiza majuku ya timu yake ya Taifa ya Burundi.


Said alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Injinia Hersi amesema:"Ataanza kuutumikia mkataba wake tarehe 15 Novemba 2020 na ni mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

"Ataripoti kuitumikia klabu baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa nchi yake inatarajiwa kucheza mechi ya pili tarehe 15 Novemba.

"Hivyo atakuwa ndani ya timu kwa nusu ya msimu huu na msimu ujao atakuwa msimu kamili na atamaliza kabisa kuitumikia timu ya Yanga," amesema.

6 COMMENTS:

  1. Walishindwa kumsajili wanasubiri awe huru wamsajili

    ReplyDelete
  2. Hilo swali niliuliza, timu bado zinaendelea kusajili? Dirisha lipo wazi?

    ReplyDelete
  3. Huyu ni mchezajibhuru hana timu....anaruhusiwa kusajiliwa sheria inaruhusu

    ReplyDelete
  4. Ila hatocheza mpaka dirisha lifunguliwe January

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic