NGAWINA Ngawina, Kocha Mkuu wa Ndanda FC amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Oktoba 13 dhidi ya Simba.
Ndanda FC ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza leo itashuka Uwanja wa Azam Complex kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ngawina amesema:" Mpira wa miguu ni mchezo wa wazi na wachezaji wangu watapambana kupata matokeo ndani ya uwanja.
"Nitawatumia wachezaji wote wale ambao wapo tayari na nina amini kwamba hawataniangusha kikubwa ni sapoti na wachezaji watapambana kutimiza majukumu ndani ya uwanja." amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment