October 13, 2020


 Mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Mbwana Samatta ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wametembelewa zaidi kwenye mtandao wa Transfer Marketing wakati wa dirisha la usajili wa majira ya Joto.

 

Kwa mujibu wa transfermarket, Samatta ametinga tatu (3) bora kwenye Orodha hiyo inayoongozwa na mchawi wa soka Lionel Messi nafasi ya pili ikichukuliwa na fundi wa mpira Cristiano Ronaldo huku ya tatu ikienda kwa Mtanzania, Captein Diego, Samatta.

 

Nafasi ya nne ikienda kwa Cavani na ya tano kwa Suarez. Cavani amekuwa akifuatiliwa kutokana na dili lake la kuelekea Manchester United wakati Suarez ni sekeseke lake na Barcelona ambalo lilihitimishwa kwa kushuhudia nyota huyo akitua Atletico Madrid.

 

Samatta amejiunga na Fenerbahce ya Uturuki katika dirisha la usajili lililofungwa wiki iliyopita akitokea katika klabu ya Aston Villa ya England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic