KINARA wa pasi za mwisho kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na nyota wa klabu ya Simba, Luis Miquissone ‘Konde Boy’ amesema kuwa amejipanga kufanya makubwa zaidi msimu huu wa 2020/21.
Akiwa amecheza mechi nne ndani ya Simba Luis amekuwa ni mtambo wa kutengeneza na kufunga mabao.
Luis amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu ambapo amehusika kwenye mabao sita kati ya 14 ambayo Simba imefunga kwenye michezo yao mitano iliyopita.
Amefunga bao moja na kutoa pasi tano za mabao na mchezo wake dhidi ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 alitoa jumla ya pasi tatu rekodi ambayo bado haijavunjwa.
Akizungumzia kiwango chake Luis alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuwa na mwanzo mzuri msimu huu, ambapo kwenye michezo mitano iliyopita nimefanikiwa kufunga bao moja na kuasisti mara tano, kwangu nimekuwa nikisema mara zote kuwa natamani kufanya vizuri kwenye kila mchezo kwa ajili ya mafanikio ya Simba.
“Kiwango nilichofanikiwa kukionyesha kwenye michezo iliyopita na ushindani wa namba uliopo kwenye kikosi vimezidi kunipa ari ya kutaka kufanya vizuri zaidi, hivyo naamini nitakuwa moto zaidi kwenye michezo ijayo baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa kumalizika,” alisema kiungo huyo raia wa Msumbiji.
Safi kabisa wafunge kandambili tarehe 7 wafukuze huyo kocha wao wanao mleta tena
ReplyDelete