October 5, 2020

 


INJINIA Hersi Said, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo amesema kuwa benchi la ufundi linabaki chini ya Juma Mwambusi ambaye alikuwa ni kocha msaidizi wa klabu hiyo.


Mwambusi alikuwa akifanya kazi chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krimpotic ambaye alifungashiwa virago vyake ndani ya Yanga Oktoba 3 muda mfupi baada ya kutoka kukiongoza kikosi chake kushinda mabao 3-0 mbele ya Coastal Union.

Hersi amesema:"Kwenye benchi la ufundi ameondolewa Zlatko peke yake, hivyo kwa sasa timu itakuwa chini ya Juma Mwambusi pamoja na wale wengine aliokuwa akifanya nao kazi.

"Kikubwa kwa sasa tunaangalia namna gani tunaweza kumpata mrithi wake ila hakuna kitakachoharibika kwani mipango inakwenda vizuri mashabiki na wadau wasiwe na mashaka taarifa watazipata muda sio mrefu."

Zlatko amekiongoza kikosi kwenye mechi tano za ligi ambapo alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons na alishinda mechi nne akifikisha jumla ya pointi 13 kibindoni.

Kwenye mechi zake zote ambazo alikuwa benchi timu yake haikupoteza mchezo.

6 COMMENTS:

  1. Mzungu kaondoka sasa timu inakabidhiwa vigagura vya kutengeneza matikeo ya tar 18

    ReplyDelete
  2. Mzungu kaondoka sasa team wanepewa mababu wandumba kuelekea tarehe 18. 18 itachezwa ndumba vs Simba sc. Kwa Nina la YESU ndumba itafeli

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona kelele zinaanza mapema hivi???
      unamtaja YESU kwenye mambo ya kinafiki??

      Delete
    2. Kwani uongo hamtumiagi ndumba/hakuna ndumba kwenye mpira wakibongo?

      Delete
  3. Senzo kashafanya yake, Leo kasema maamuzi yaliyofanyika ni sahihi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic