October 12, 2020

 


KESHO, Oktoba 13 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ndanda FC.


Ndanda inashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka msimu wa 2019/20 mchezo wake wa kwanza ililazimisha sare mbele ya African Lyon Uwanja wa Uhuru.


Itacheza mchezo huo wa kirafiki na Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wakiwa nafasi ya pili na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano ndani ya ligi.

Uwanja wa Azam Complex utakuwa na kazi ya kuhimili vishindo vya nyota wa timu hizo mbili ambapo muda itakuwa ni kuanzia saa 11:00 jioni.


Kiingilio kwenywe mchezo huo kwa VIP ni shilingi 7,000, (buku saba) na mzunguko ni buku tano, (5,000).



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic