October 10, 2020


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kwa sasa yeye maisha yake yapo ndani ya timu hiyo hivyo hawezi kuzungumzia ishu yake ya kutakiwa na Klabu ya Yanga.


Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya atakayebeba mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 baada ya kuongoza kikosi chake kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara na alishinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.


Wakati wa kumtafuta mrithi wa Luc Eymael jina lake lilikuwa linatajwa kuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kuibukia ndani ya timu hiyo kukaa kwenye benchi la ufundi ila nafasi yake ilichukuliwa na Krmpotic ambaye naye ameshafutwa kazi.


Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa ameshapewa kandarasi ndani ya Kagera Sugar hivyo hawezi kuzungumzia suala lake na Yanga.


"Mimi kwa sasa nimeajiriwa ndani ya Kagera Sugar hivyo huku maisha yangu ndipo ambapo yapo, kuhusu kufanya mazungumzo na Yanga hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa.


"Kikubwa ambacho ninakifanya ni kuona  kwamba timu yangu inafanya vizuri kwenye mechi zote ambazo tutacheza na maisha yaendelee," amesema.


Kagera Sugar kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi tano imeshinda mechi moja, sare moja na kupoteza mechi tatu na ina pointi nne. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic