October 10, 2020


 UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa umekaa kikao na Kocha Mkuu wa timu hiyo Hitimana Thiery kuzungumza naye kuhusu mwendo wao wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.


Namungo FC ambayo msimu huu ina kazi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ambayo ni ya Kombe la Shirikisho imecheza mechi tano za ligi imeshinda mbili na kupoteza mechi tatu.


Safu yake ya ulinzi imeruhusu kufungwa mabao matatu huku wao wakifunga mabao mawili yaliyofungwa na Bigirimana Blaise.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi sita na vinara ni Azam FC wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi tano na kushinda zote.

Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu amesema kuwa kwa namna ambavyo kikosi chao kinakwenda kwenye ligi imewalazimu kukaa chini kuzungumza na benchi la ufundi kujua tatizo lilipo.


"Tulianza kukaa kikao na uongozi wenyewe kisha tulimuita kocha tukazungumza naye tukiwa na benchi lote la ufundi pamoja na viongozi kisha baadaye tulizingumza na kocha mwenyewe ili kujua tatizo lipo wapi.


"Kweli hatujaanza vizuri msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita na hii ni sababu kwamba msimu huu maandalizi yamekuwa mafupi kutokana na janga la Virusi vya Corona.

"Jambo hili sio kwetu pekee bali hata wengine pia walikutana na jambo hili ila tupo tayari na tunapambana kuona namna gani tunaweza kurejea kwenye ubora wetu," amesema.



2 COMMENTS:

  1. Waulize KMC,hata Hiyo michuano ya Africa mtapigwa nje ndani tunajua.Halafu mtaponea chupuchupu kushuka daraja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo uungwana huo tunanitani kutiana moyo. Mwenziyo smifanya vzr siyo kumtupia nawe bali kumtia moyo Ili afanye vzr zaidi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic