MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Mancheter United, Ed Woodward anajiandaa kumfuta kazi Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer kama ataendelea kupata matokeo mabovu ndani ya kikosi hicho kwa mujibu wa ripoti.
United kwa sasa inapambana kuunda kikosi kipya cha kazi ambacho kitawapa matokeo chanya ndani ya Ligi Kuu England ambapo kwenye mechi tatu za mwanzo imeonekana ikipata matokeo yasiyopendeza.
Jumapili iliyopita ilikubali kichapo cha mabao 6-1 ikiwa Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Spurs jambo ambalo limeongeza presha kubwa kwa Solskjaer kuondolewa ndani ya kikosi hicho na jina ambalo linatajwa kupewa mikoba yake ni Mauricio Pochettino, kocha wa zamani wa Spurs.
Kwa mujibu wa habari za ndani zinaeleza kuwa Woodward ameandaa ujumbe maalumu kwa ajili ya kumuondoa kocha huyo kipenzi cha aliyekuwa kocha wa zamani wa timu hiyo alipokuwa akicheza chini ya Sir Alex Ferguson.
Pia amekasirishwa na suala la timu hiyo kushindwa kupata saini ya winga Jadon Sancho anayekipiga ndani ya Borussia Dortmund jambo analoamini linalofanya wapate tabu kupata matokeo kwenye mechi zao walizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment