October 13, 2020


MWENYEKITI wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Wakili Kichere Mwita Waissaka amesema kuwa suala la mchezaji wa Simba, Bernard Morrison lililowasilishwa kwenye kamati hiyo halijasikilizwa kwa kuwa mchezaji huyo alituma wawakilishi.


Waissaka amesema kuwa yapo mambo ambayo yanapaswa kuwakilishwa na wawakilishi lakini kwenye suala la Morrison ambalo ni la kimaadili alipaswa awepo yeye mwenyewe ili aweze kuyajibu maswali mengine ambayo hayawezwi kujibiwa na wawakilishi. 

Waissaka amesema:- "Mashtaka dhidi ya Bernard Morrison kifupi ni kwamba mlalamikiwa hakufika mwenyewe alitoa udhuru ni sababu iliyofanya kamati ikashindwa kuskiliza hukumu kwa kuwa alisema yupo na Klabu ya Simba.


"Hata hivyo alituma wawakilishi wawili ambao ni wanasheria hata hivyo kamati iliona kwamba ni haki mlalamikiwa mwenyewe awepo hivyo kamati iliamua kuahirisha suala hilo.

"Sababu kuna maswali mengine yalipaswa yajibiwe na  mchezaji mwenyewe na sio wawakilishi hivyo wangeshindwa kujibu.

"Pia kamati iliarifiwa kwamba suala la Morrison limeripotiwa kwenye mahakama ya usuluhishi ya Fifa lakini ieleweke pia iliyokatiwa rufaa ni kwenye masuala ya usajili kwenye masuala ya maamuzi ya usajili ambao wamekatiwa rufaa ni kamati ya usajili kwenye Cas, chombo hiki kipo Uswisi.


"Suala lililoletwa mbele ya kamati yetu ni la maadili isipokuwa masuala ya usajili yameripotiwa huko mbele kwenye kamati ya Cas." amesema.


Morrison yupo kwenye mvutano na Klabu yake ya Yanga kwenye suala la mkataba wake ambapo Yanga waajiri wake wa zamani wanaeleza kuwa alikuwa na mkataba wa miaka miwili huku yeye akidai kuwa alikuwa na kandarasi ya miezi sita.


Sakata hilo lilisikilizwa TFF na aliweza kushinda kwa kile kilichoelezwa kuwa mkataba ulikuwa na mapungufu kati yake na waajiri wake jambo lililomfanya awe huru kuchagua timu anayokwenda kuitumikia.


Kutokana na majibu hayo Yanga walieleza kuwa wanakwenda Cas kukata rufaa ili kupata haki juu ya mchezaji huyo.


10 COMMENTS:

  1. Tuletee mambo ya msingi siyo upuuzi huo

    ReplyDelete
  2. Viwanja ni mali ya watanzania wote sio TFF au CCM aacheni uhuni wenu

    ReplyDelete
  3. Yanga jamani, kesi mara IPO tff mara IPO cas mbona tunakosa welekeo jamani. Tufuate kipi?

    ReplyDelete
  4. Jamani naomba kuelewashwa kuhusu mkataba wa MORRISON anayetakiwa kulalamika MORRISON AU TIMU YA YANGA?.Huo mkataba anayekosa haki zake ni MORRISON au Yanga kutokana mkataba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili ni kiporo cha mashtaka ya Kamati ya Sheria dhidi ya Morrison kwenda kwenye Kamati ya Maadili. Yalitolewa sambamba na shitaka alilohukumiwa Manara na Hanspope, ila la Morrison liliwekwa kiporo. Ni tofauti na mashtaka yaliyoibuliwa juzi na Mwakalebela dhidi ya mkataba wa Simba na Morrison

      Delete
  5. Afadhali wewe umenielewesha !!! Acha utopolo waendelee kuzulula mahakamani utadhani Wana jinai

    ReplyDelete
  6. Hawana akili hao ndio mana wakaitwa KANDAMBILI

    ReplyDelete
  7. Mafara nyie mwamedi na mke wake manara wanawashusha daraja mwaka huu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic