October 4, 2020

 



MTIBWA Sugar leo Oktoba 4 imeshindwa kumaliza Biashara mapema Uwanja wa CCM Kirumba baada ya kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo bao la Biashara United lilifungwa na mshambuliaji wao namba moja, Kelcin Friday dakika ya 9.

Bao hilo linamfanya Friday afikishe jumla ya mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa bao lake la kwanza alifunga mbele ya Mwadui FC wakati wakishinda Uwanja wa Karume.

Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila kutunguliwa baada ya ule wa wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri mbele ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic