OKTOBA 11 mashabiki wa Tanzania, wataweka kando tofauti zao zote kisha kazi itakuwa ni moja tu kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars
Ni mchezo wa kirafi uliopo kwenye kalenda ya Fifa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kuambana kupata ushindi.
Burundi ina kumbukumbu ya kutolewa na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu Kombe la dunia uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 8/2019 zama hizo ulikuwa unaitwa Uwanja wa Taifa sasa umebadilishwa jina.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore nchini Burundi, timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hata ule wa marudiano pia dakika 90 ngoma ilikuwa ni 1-1, Stars ilishinda kwa penalti 3-0 na shujaa alikuwa Juma Kaseja.
Championi Ijumaa linakuletea sababu saba zitakazokufanya Mtanzania uipe sapoti timu ya Taifa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa namna hii:-
Uzalendo
Taifa ni letu sote na timu ni yetu sote hivyo kujitokeza kwa mashabiki kwa wingi Uwanja wa Mkapa ni uzalendo na kuonyesha kujali.
Wachezaji waliotusua nje ya Bongo
Soka la Bongo linazidi kukua na matunda yake yanaonekana hata sasa. Kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, kuna wachezaji 6 ambao wanacheza nje ya Bongo.
Fenerbahce ya Uturuki na tayari ametupia mabao mawili kibindoni kwa timu yake akiwa amecheza mechi mbili. Alijiunga na timu hiyo kwa mkopo msimu huu akitokea Klabu ya Aston Villa ambayo inashiriki Ligi Kuu England.
Akiwa ndani ya Aston Villa pia alitupia mabao mawili, moja ilikuwa kwenye Ligi Kuu England alipocheza mechi 14 na moja kwenye Kombe la Carabao. Mkononi anashikilia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England ambayo ni ligi pendwa duniani.
Himid Mao, zao la Azam FC kwa sasa yupo ndani ya ENPPI ya Misri, Simon Msuva aliitumikia Yanga yupo Diffaa El Jadida pamoja na Nickson Kibabage zao la Mtibwa Sugar. Ally Msengi yupo Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Thomas Ulimwengu yupo TP Mazembe ya Congo.
Uwanja wa Mkapa
Ni mechi ya kwanza ndani ya 2020/21 baada ya jina la uwanja kubadilishwa kutoka Uwanja wa Taifa mpaka kuitwa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Oktoba 11 itapigwa mechi ya kwanza kwa timu ya Taifa ya Tanzania.
Rekodi itakuwa inasakwa kwa timu zote mbili kuona nani atakuwa mbabe kwa nyota hawa wawili ndani ya dakika 90.
Ujirani mwema
Nchi hizi zote mbili zipo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Maana yake ni kwamba tabia pamoja na hulka za wachezaji zinaendana hakuna tofauti katika maisha ya soka.
Hata kwenye upande wa ajira bado kumekuwa na ujirani mwema kwa wachezaji kutoka Burundi kufanya kazi pamoja na makocha pia kufanya kazi ndani ya Bongo. Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije ambaye yupo ndani ya Timu ya Taifa ya Tanzania yeye ni raia wa Burundi ila yupo kikazi ndani ya ardhi ya Tanzania akiwa ni Kocha Mkuu. Hivyo kwa upande wa ujirani tupo nao vizuri ila yote yatawekwa kando kisha kazi itakuwa uwanjani.
Rekodi za makipa
Makipa watatu ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa msimu wa 2020/21 rekodi zao wote ni kali. Hili pia lazima liongeze nguvu kwa mashabiki kujua nani atakayepewa dhamana ya kukaa langoni.
Ndayiragije amemuita, David Kissu kutoka Azam FC yeye rekodi zake zinaeleza kuwa akiwa amecheza mechi tano za Ligi Kuu Bara, amefungwa mabao mawili na mechi nne hajafungwa.
Metacha Mnata wa Yanga pia naye yumo. Amecheza mechi nne za ligi na zote hajafungwa.
Aishi Manula wa Simba naye ameitwa pia, amecheza mechi tano na amefungwa mabao mawili hajafungwa mechi tatu.
Presha ya Yanga v Simba hakuna
Utani wao unawekwa kando sasa inakuwa kazi juu ya kazi. Awali presha ilikuwa kubwa kwa sababu watani hawa walikuwa wakimaliza kibarua Oktoba 11 wangekuwa wamebakiwa na siku sita kukutana Oktoba 18. Ila taarifa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) imeeleza kuwa mechi hiyo itachezwa Novemba 7.
Simba ina wachezaji saba ndani ya Stars ambao ni Aishi Manula, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, John Bocco, Mzamiru Yassin na Said Ndemla.
Yanga ina wachezaji wanne ambao ni Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto, Ditram Nchimbi na Feisal Salum.
Wachezaji wa Burundi wanaokipiga Bongo
Kwenye timu ya Burundi kuna jamaa watatu maisha yao ya soka kwa sasa yapo ndani ya Bongo. Kipa wao namba moja, Jonathan Nahimana yeye yupo Namungo kwa mkopo akitokea Klabu ya KMC, Bigirimana Blaise na Styve Nzigamasabo wote wapo zao ndani ya Namungo.
Wanalitambua soka la Bongo jambo ambalo litaongeza ushindani mkubwa.
Nawatakia wachezaji wetu afya njema na ushindi mwema Taifa stars oyeeeee twende tukaonyeshe uzalendo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa piga keleleee watanzania wote
ReplyDelete