SAID Ndemla, kiungo wa Simba amesema kuwa hana hofu yoyote ile ndani ya kikosi hicho bado anaamini ana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa uwezo anao.
Ndemla ni miongoni mwa wachezaji ambao wameitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Star ambayo inamchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi Uwanja wa Mkapa.
Mchezo huo unataraiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 leo Oktoba 11 na utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kujuana katika falsafa pamoja na ujirani wake.
Ndemla ndani ya Simba amekuwa adimu kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba hasa kwenye nafasi ya kiungo ambayo anacheza nafasi ya ukabaji sawa na Jonas Mkude ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.
Kiungo huyo amesema:"Uwezo ninao na kikubwa ambacho kitanifanya niweze kufikia malengo niliyojiwekea ni juhudi pamoja na kujituma sina mashaka katika hilo."
Simba ikiwa imecheza mechi tano za ligi, Ndemla amecheza mechi mbili ambazo ni sawa na dakika 180.
0 COMMENTS:
Post a Comment