MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Pierre- Emerick Aubameyang ameendelea kuwashtua wengi kutokana na kiwango ambacho amekuwa akikionyesha msimu huu.
Staa huyo ambaye misimu miwili iliyopita alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa timu hiyo kwa sasa mambo yake yanaonekana kuwa magumu akiwa na ukame mkubwa wa mabao.
Pamoja na kwamba anategemewa na timu hiyo wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kuanzia aliposaini mkataba mpya wa miaka mitatu na timu hiyo ameshindwa kuwika.
Kwenye mchezo waliolala kwa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa wikiendi iliyopita hakufanikiwa kupiga shuti hata moja langoni kwa dakika zote alizocheza ikiwa ni rekodi kwake kwa michezo ya nyumbani.
Takwimu zinaonyesha kuwa ana wastani mbovu kwenye ligi hiyo msimu huu tafauti na misimu kadhaa iliyopita.
TAKWIMU
Mabao aliyofunga msimu huu: 2
Mashuti aliyopiga langoni :10
Michezo aliyocheza ya ligi: 7
Mabao aliyofunga michuano mingine: 2
Mabao aliyofunga msimu uliopita kwenye ligi: 22
Mabao ya jumla aliyofunga msimu uliopita: 29
Michezo aliyocheza msimu uliopita:44
Mabao aliyofunga jumla akiwa na Arsenal: 74
Michezo jumla aliyocheza:118
Mabao jumla kwenye timu zote: 270
Michezo jumla aliyocheza: 514
Makombe aliyotwaa: 6
0 COMMENTS:
Post a Comment