GWIJI wa Klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil, Rivaldo amesema kuwa klabu yake hiyo ya zamani inapaswa isajili washambuliaji wawili kwa namna yoyote ile ikiwa wanahitaji kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Nyota huyo amesema kuwa itakuwa ni habari njema kwa mashabiki pamoja na wachezaji ndani ya Nou Camp ikiwa watapata washambuliaji wazuri kwa kuwa nyota wao aliyekuwa anakuja vizuri ni majeruhi hivyo anapaswa apatikane mbadala wake.
Kwa sasa Ansu Fati ambaye ni mshambuliaji chipukizi anasumbuliwa na majeraha yatakayomfanya awe nje kwa muda wa miezi minne jambo ambalo linawapa ugumu Barcelona kumpata mbadala wake na Lionel Messi hajawa kwenye ubora wake msimu huu.
Fati mwenye miaka 18 aliumia mguu Novemba 7 wakati timu yake ikishinda mabao 5-2 dhidi ya Real Betis kwenye mchezo wa La Liga.
Rivaldo amesema kwa namna ushindani ulivyo mkubwa ndani ya La Liga pamoja na Ligi ya Mabingwa ulaya ni lazima kwa timu hiyo kufanya usajili wa washambuliaji ili kupata matokeo ndani ya uwanja.
"Nadhani Barcelona wanatakiwa wapate mshambuliaji mwingine zaidi ya Asu Fati na ilipaswa awepo hata kabla ya kupata majeraha, kwa sasa wataanza kupambana kupata matokeo.
"Ronald Koeman amekuwa akiwaamini vijana ana kazi ya kuweza kuongoza kikosi katika mechi zake nyingine zijazo kwa kupambania ushindi hivyo anahitaji kupata saini ya mshambuliaji mmoja ama wawili," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment