November 8, 2020

 


IMEELEZWA kuwa sare ya jana kwa Simba kuipata Uwanja wa Mkapa ya kufunagana bao 1-1 dhidi ya Yanga ilitokana na baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho kucheza chini ya kiwango.


Wachezaji wanaotajwa kucheza chini ya ni pamoja na kiungo namba moja wa kutengeneza mabao ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21, Luis Miquissone akiwa nazo sita, Clatous Chama mwenye pasi tano za mabao na Rarry Bwalya mwenye pasi moja ya bao.


Wengine ni pamoja na Shomari Kapombe ambaye jana alisababisha kona iliyoleta bao la kusawazisha kwa Simba lililofungwa na Joash Onyango na nahodha msaidizi Mohamed Hussein,'Tshabalala' ambaye alipewa tuzo ya mchezaji bora na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda.


Taarifa zimeeleza kuwa mmoja wa viongozi ndani ya Simba amebainisha kuwa wachezaji hao walicheza chini ya kiwango jambo ambalo limesababisha washindwe kupata ushindi kwenye Dar Dabi.


Mara baada ya mchezo wa jana Novemba 7 ambapo Yanga ilipata bao kupitia kwa Michael Sarpong Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck aliweka bayana kuwa walistahili kupata ushindi kwa namna ambavyo walicheza.


"Wachezaji walipambana kwenye kusaka matokeo ila haikuwa bahati yetu, licha ya kwamba tuliceza vizuri na tulistahili ushindi kuna matatizo ambayo yametufanya tushindwe kupata matokeo kwa kushindwa kutumia nafasi ambazo tulizipata," amesema.


Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 20 na watani zake wa jadi wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 24.

5 COMMENTS:

  1. Mwanzo wa chokochoko ni shutuma za kijinga kama hizi.Lazima tukubali kuwa wachezaji walipambana kiasi cha uwezo wao na pia tukumbuke siku hazifanani

    ReplyDelete
  2. Upuuuzi sasa Hans pope, kwanza lazima ashukuru kwa kupata sare maana kwa YANGA hii jitu litakufa mapema tu

    ReplyDelete
  3. Acheni upumbavu vijana walipambana hadi tone lao la mwisho au mmetumwa kutuchanganya?!!!! mpango wenu feki kamwe hautafulu KIMA NYIE

    ReplyDelete
  4. Hawa viongozi washenzi wanataka kuwavuruga wacheza,sote tuliona wachezaji wakipambana,Hans rudi magereza hii ndio inafanya wachezaji kwenda team pinzani,hao ni professional players acheni kuvuruga team.

    ReplyDelete
  5. Hiyo ni sare, shutuma kibao je,mungefungwa si mungeuwana? Wafukuzeni hao ili musajili wengine wapya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic