VINARA wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wameweka bayana kuwa msimu huu wana jambo lao ambalo wanahitaji kulitimiza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, Azam FC imekusanya pointi 25 kibindoni na kufunga mabao 18 katika mechi 10 ambazo wamecheza.
Mchezo mmoja wamepoteza ugenini kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Ina kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya KMC Novemba 21, Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na watapambana kupata matokeo kwenye mechi zao zijazo.
"Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wanajua kwamba kinachohitajika ni ushindi ile presha waliyokuwa nayo mwanzo kwa sasa hawatakuwa nayo kwa kuwa wameonja ladha ya kupoteza, ladha ya ushindi na sare.
"Bado mapambano yanaendelea na kupitia mechi za kirafiki tutaongeza zaidi hali ya kujiamini kwa wachezaji na kuwa imara kwa mechi zijazo sisi tuna jambo letu," amesema.
Wanajambo lao kweli ngoja wakutane na mnyama ndio tutajua wanajambo lao kweli.
ReplyDelete