MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wana kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union Novemba 21.
Mchezo huo wa raundi ya 11 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha saa 10:00 jioni baada ya uwanja wa Mkwakwani uliopo jijini Tanga kufungwa.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho wanahitaji kwenye mechi zao zote za ligi ni kupata pointi tatu muhimu ili kufikia malengo.
"Ikiwa unahitaji kuwa bingwa kazi huwa inakuwa moja kupata matokeo kwenye mechi zote utakazocheza ndivyo itakavyokuwa kwenye mechi zetu zijazo.
"Ninajua kwamba ushindani ni mkubwa lakini kikosi kipo tayari na wachezaji wanajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo chanya hivyo kikubwa watupe sapoti," amesema.
Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 10 na pointi 12 kibindoni.
Ndani ya michezo kumi umepoteza miwili na na kudraw miwili ubingwa kazi sana
ReplyDelete