November 28, 2020

 


KIKOSI cha Azam FC kimewasili Mara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ya Mara maarufu kama wanajeshi wa mpakani.


 Mchezo huo utachezwa Jumatatu, Novemba 30 Uwanja wa Karume na utakuwa ni wa Kwanza kwa Kaimu Kocha Mkuu,  Vivier Bahati kukaa Kwenye benchi.


Bahati amepewa mikoba ya Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 baada ya kupoteza mchezo mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa Bahati ataongoza timu hiyo Kwenye mechi mbili ya Kwanza itakuwa hii dhidi ya Biashara United na ya pili itakuwa dhidi ya Gwambina FC.

3 COMMENTS:

  1. Kwa Biashara United kazi mnayo kupata ushindi maana wanakuwa wagumu Sana nyumbani na wametoka kufungwa bao 3 wiki iliyo pita.

    ReplyDelete
  2. Kichapo cha tatu mfururizo kinawahusu hawezi toka salama pale na majeruhi aliyonayo nampa pole kocha mpya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic