November 29, 2020

 


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa nyota wake Bruno Fernandes ni kama Cristiano Ronaldo. 

Hivi karibuni baada ya nyota huyo kufanya vizuri ndani ya United amekuwa akifananishwa na Ronaldo ambaye aliwahi kuitumikia timu hiyo na wote ni raia wa Ureno.

Fernandes amefunga jumla ya mabao 21 katika mechi 35 ndani ya United tangu atue hapo Januari mwaka huu akitokea Sporting Lisbon na ana jumla ya asisti 15.

Solskjaer amesema:"Fernandes ni kama Ronaldo yeye amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji kuwahamasiha wapambane zaidi wakiwa ndani ya uwanja hilo ni jambo nzuri," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic