November 13, 2020

 




KIUNGO wa Klabu ya Yanga, Mukoko Tonombe, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.


Mwezi huo wa Oktoba, Yanga ilicheza michezo minne, ikiwa ndiyo timu iliyoshinda michezo yake yote na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 18.

 Yanga ilizifunga Coastal Union 3-0, Polisi Tanzania 1-0, KMC 1-2 na Biashara United, 0-1 ambapo Mukoko alitoa mchango mkubwa katika ushindi huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao moja dhidi ya Polisi Tanzania.

Mukoko amemshinda nyota wa Azam FC, Prince Dube na mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali, ambapo Dube aliiongoza Azam kubaki kileleni baada ya kuvuna pointi 10 katika mwezi huo, ikishinda tatu, sare moja na kupoteza mmoja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za usaidizi wa mabao.

Kwa upande wa Meshack aliiongoza Gwambina kupata pointi nane ikishinda michezo miwili, sare mbili na kupoteza mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi ya 14 akiifungia timu yake mabao manne.

3 COMMENTS:

  1. Kwa vigezo gani au ndo kukurupuka homeboy hapa kutoka mtowisa sumbawanga

    ReplyDelete
  2. Na bdo atazichuka sana he zo tuzoooo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic