KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.
Kaze amewashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote.
Yanga chini ya Kaze ilizifunga Polisi Tanzania 1-0, KMC 1-2 na Biashara United 0-1 na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mmoja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.
Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mmoja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment