LEO saa 11:00 ni muda wa mechi kali yenye historia kwenye soka la Bongo ambapo mabingwa watetezi Simba watavaana na mabingwa wa kihistoria Yanga.
Hii itakuwa mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana msimu huu ambapo Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 19 baada ya kufanikiwa kucheza michezo 9 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 23 baada ya kucheza michezo 9.
Katika mchezo wa Jumamosi, Simba ndiyo wanaonekana kuwa kwenye presha kubwa zaidi kutokana na matokeo ambayo wameyapata siku chache zilizopita baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Prisons walipochapwa bao 1-0 na dhidi ya Ruvu Shooting walipolala kwa bao 1-0.
Hali hii inaonyesha dhahiri kuwa kama Simba watapoteza mchezo wa leo dhidi ya Yanga basi mambo yao yanaweza kuwa magumu zaidi kwa kuwa Yanga watakuwa wamewaacha kwa pointi 7.
Ikiwa itakuwa hivyo mambo yatakuwa magumu kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi.
Lakini pia Simba wapo kwenye presha kubwa baada ya kuonekana kuwa na wachezaji muhimu wenye majeraha tofauti na watani wao.
Simba inatajwa kuwa itamkosa Chris Mugalu na Meddie Kagere na hawa wameonekana kuwa nguzo muhimu sana kwao,wanachosubiri kwa sasa ni kuhakikisha wanamlinda staa wao John Bocco awe fiti kwa asilimia 100 kabla ya mchezo huo
hali hii imewafanya Simba wapangue kikosi chao na wanaonekana kuwa wana pigo kubwa kwao tofauti na Yanga ambao wanaonekana kuwa imara kwa asilimia 100.
Yanga wao leo watamkosa kiungo wao Carlos pamoja na Mapinduzi Balama.
Mugalu sio majeruhi na anaweza kucheza acha porojo
ReplyDeleteAlishapona mechi na kagera aliingia kipindi cha pili kupasha misuli
ReplyDelete