SALUM Abubakari, nyota wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani wa Ligi Kuu Bara jambo ambalo linawafanya wawe imara wanapokuwa ndani ya uwanja.
Novemba 5, Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC na imekwea kileleni ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 za ligi.
Ikiwa imetupia jumla ya mabao 18, Sure Boy amehusika kwenye mabao mawili akifunga bao moja na kutoa pasi moja ndani ya Azam FC na zote ilikuwa ni Uwanja wa Azam Complex.
Nyota huyo amesema:"Kila mchezaji anapenda kuona timu ikipata ushindi na mwisho wa siku tukishinda tunafurahi pamoja na hili linawezekana kutokana na sapoti ambayo tunaipata kutoka kwa mashabiki," .
0 COMMENTS:
Post a Comment