November 7, 2020


YAMEBAKI masaa leo Novemba 7 kabla ya watani wa jadi Yanga na Simba kukutana Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu, mabingwa watetezi Simba wameweka bayana mitambo ya kazi itakayowamaliza wapinzani wao.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na hasira za kulipa kisasi baada ya kupoteza pointi nne msimu uliopita kwenye dabi ya Kariakoo baada ya mchezo wa kwanza Januari 4 kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na ile ya Machi 8 Simba kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameliambia Spoti Xtra kuwa hawana mashaka na mchezo huo kwa kuwa wana wachezaji wengi wenye ubora ndani ya uwanja jambo linalowapa hali ya kujiamini.

“Kila kitu kipo sawa na ukitazama kikosi kina Chama,(Clatous), Bwalya,(Larry), Luis,(Miqussone), Mugalu,(Chris) sasa hao wenzentu tutakapokutana nao sijui itakuaje.

“Sisi ni mabingwa watetezi na tuna malengo ya kutetea taji hili na kanuni ni moja ili uwe bingwa unatakiwa ushinde mechi zako, hivyo lazima tupambane kupata pointi tatu uwanjani, mashabiki watupe sapoti,” alisema Manara. 

7 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Ni kawaida kutunga habari sijajua wanatuchukuliaje hawa wandishi wa hii blog.

      Delete
  2. Simba leo wanapigwa bao mbili bila majibu. Bora sven aende na mabegi yake uwanjani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mawazo ya kiutoplo Kama ulivyo utopolo. Leo ukuta wenu utopolo tunauyeyusha Kama udongo unavyokumbana na dhoruba ya maji

      Delete
  3. Ynga msiende uwanjani mvua imenyesha huko Dar

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic