LEO nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuchezwa fainali ya mashindano ya Cosafa kati ya Tanzania na Zambia.
Kwenye mchezo wa leo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa yupo nyota mmoja mwenye uwezo wa kucheka na nyavu anaitwa Asha Masaka ambaye amesema kuwa malengo yake ni kufunga mabao mengi kila apatapo nafasi.
Tangu ameanza kucheza timu ya Taifa, Masaka amefunga jumla ya hat-trick nne kwenye michuno mitatu tofauti, kwa upande wa klabu amefunga hat-trick sita na kumfanya awe na jumla ya hat-trick 10 kwenye msimu wa 2018- 19 na 2019-20.
Amefunga hat trick mbili kwenye Cosafa ya mwaka huu, alifunga nyingine kwenye Cosafa ya U20 mwaka jana dhidi ya Eswatin, akafunga tena kwenye mashindano ya Cecafa yaliyofanyika mwaka jana nchini Uganda.
Kwenye Cosafa alifunga dhidi ya Djibouti, kisha akafunga nyingine mbele ya Burundi, kwenye michezo ya kufuzu Kombe la Dunia, michezo yote ikichezwa mwaja jana. Kwa upande wa klabu, alifunga dhidi ya Baobab Queens, Panama Queens na Mapinduzi Queens, hii ilikuwa ni 2018-19. Msimu wa 2019-20 alifunga dhidi ya JKT Queens, TSC Academy na Panama Queens.
Asha amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.
Gem hiyo imeisha kwa Tanzania kuibuka na ushindi wa penalt 4 kwa 3 mara baada ya sare ya 1–1 ndani ya dkka 90
ReplyDeleteAhsante sana Mzalendo kwa kutuliza maana nilikuwa nauliza uliza mechi itakuwa saa ngapi
DeleteDu!Tulisawazisha dakika za nyongeza kwa penalt,vijana walicheza mpira mkubwa sana,wananikumbusha enzi za super eagle mwaka 1998.
ReplyDelete