KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amesema kuwa kupoteza mchezo mbele ya Tunisia ni somo watapambana kwenye mchezo wa marudio kupata matokeo chanya.
Stars ikiwa ugenini usiku wa kuamkia leo ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya wayeyushe pointi tatu jumlajumla ugenini kwenye mchezo wa kufuzu Afcon 2022 nchini Cameroon.
Ikiwa ipo kundi J, imebakiwa na pointi zake tatu baada ya kucheza mechi tatu na wapinzani wao Tunisia wanafikisha pointi tisa kwa kuwa hawajapoteza mchezo kati ya mitatu ambayo wamecheza.
Kocha huyo amesema:"Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani, tunarudi nyumbani tuna amini tutafanya vizuri na kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa marudio," .
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa na mashabiki wataruhusiwa kuingia ni asilimia 50 ikiwa ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Kwenye mchezo wa ugenini hakukuwa na mashabiki walioingia uwanjani baada ya Caf kuzuia uwepo wa mashabiki.
Tutafika tu
ReplyDelete