November 19, 2020


 SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), linataka kuilipa Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi Kuu England kiasi cha pauni milioni 2 ambazo ni zaidi ya bilioni sita.


Fedha hizo ndefu ni kwa ajili ya malipo ya mshahara wa beki wao matata, Joe Gomez ambaye aliumia kwenye timu yake ya Taifa ya England ilipokuwa kwenye mazoezi na anaweza kukaa nje kwa muda mrefu.



Beki huyo ambaye aliumia goti analipwa pauni 80,000 kwa wiki akiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mkwanja mrefu ndani ya timu hiyo.


Fedha hizo zitalipwa na Fifa kwa kuwa wachezaji wa England wapo kwenye mradi wa msaada wa shirikisho kubwa la soka duniani lakini wakiwa na bima ambazo zinasimamiwa na Fifa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic